
siku kadhaa zilizopita takribani mwezi sasa baada ya simu yangu aina ya infinix hot 4 lite screen yake kuonesha michirizi ya kuvuja kwa wino hii ilitokana na kutokuwa nimeiwekea screen protector baada ya kuanguka katika barabara ya lami iliweza kuonesha mchirizi mdogo tu siku hadi siku mchirizi ulizidi kuongezeka ikafanya baadhi ya sehemu katika screen ya simu kutokuonekana kabisa na baadhi ya namba hata pindi ninapokua napata ujumbe mpya au kuandika mara nyingi naicopy ujumbe huo na paste tena na kuanza kuufuta huku nikiwa nasoma hii kidogo ilinipa usumbufu zaidi licha ya kuwa nimeizoea sana simu yangu katika masuala ya uandishi sikuwa napata shida sana.
Wazo jipya likaniijia nikaamua niingie katika playstore na kupakua application moja nayoitwa ROTATION CONTROL hii inaniwezesha kuigeuza screen ya simu yangu kila upande niutakao ukiachana na ile ya kawaida ya nyuzi 90 na nyuzi 180.. tatizo halikua limemalizika sana maana kuna sehemu kadhaa katika simu pianikawa sizioni kutokana na upande mmoja wino kusamba zaidi
Sikuwezesha kujutia sana gharama ya kuinunuia simu maana mimi si mtu wa kuanza kujilaumu sana sipo hivyo kabisa
Wazo jipya likaniijia tena ‘’nina laptop yangu kwanini nisiwe naitumia kuidisplay simu” sikusita sana maana nilikua nahuitaji mkubwa sana isitoshe vitu kadhaa nimevisave kati ka simu yangu na application mbalimbali muhimu ambazo zina run kwa android device only..
Nikapakua application moja inaitwa APOWER hii inakuwezesha kudisplay simu kwa njia mbili njia ya kuunganisha simu na computer yako kwa Wi-FI njia ya pili ni ya kutumia USB WIRE njia zote ni nzuri pia ila kwa kutumia usb wire itakuwezesha kutumia simu yalo kupitia computer kama unavyoitumia simu kawaida mfano unaweza ukaandika kupitia computer maelezo mengine kuhusu app hizi ambazo unabidi uziweke katika simu yako nyingine unaidownload software yake lwe katika computer yako nitaaelezeaa katika andiko lijalo
Nini cha muhimu na cha kuzingatia kabisa
Kwanza unabidi uiwezeshe simu yako katika setting zifuatavyo ili ikuwezeshe kuinganisha na external device kama computer njii hii ni ya ku ENABLE USB DEBUGING setting hii utaipata katika simu yako kwa hatua zifuatavyo Nenda sehemu ya setting yako ya simu shuka chini hadi uone maneno haya ABOUT PHONE
BONYEZA hapo hapo nenda moja kwa moja mpaka sehemu ilioandikwa BUILD NUMBER bonyeza mara 7 mpaka uone maneno kwa screen yanaosema NOW YOU ARE DEVELOPER
rudi nyuma sehemu ya ABOUT PHONE juu yake kutakua na maneno haya DEVELOPER OPTIONS bonyeza apo
Weka kama jinsi nilivyoweka hapo katika picha ya simu hapo juu. Kufikia hapo utakua umemaliza hivyo basi ukiwa umeziweka app hizo za kuwezesha simu yako kuonekana katika screen kioo cha computer…
Labda nidokeze kidoko tu mfano kwa zile simu ambazo power button(kile kitufe cha kuzima na kuwashia simu) kikiwa kimeharibika unaweza ukaiwasha simu kwa kuconnect kwa wire wa usb katika computer hata pia ku unlock simu yako na kucopy mafaili yako yote ya simu pamoja na namba andiko lijalo nitaelezeaa zaidi namna utakavyoitumia na kuiweka katika simu yako na computer application hizi pamoja na softwares zake…
applicaion hizo ni baadhi tu?
ReplyDelete