
Kwajina Anaitwa St. Dionysius Exiguus(Dionysius the humble) tamka Dionisi. Kazaliwa mnamo mwaka 470 na kufariki mwaka 544 A.D, kazaliwa ukanda wa Scythia minor ambapo kwasasa ni Dobruja ipo katikati ya Romania na Burgaria. Alikua ni mtawa Cythian ambapo alikua mtaalamu wa Theology. Mwaka wa 5 alishi Rumi ambapo alijifunza namba za Roman Curia na kuzitafdiri toka kwenye Kigiriki kwenda Kilatini.
Anakumbukwa kwa kugundua Matumizi ya AD baada ya kufanya Calculations kuhusu mwaka aliozaliwa Yesu ambapo inatumika kwenye kalenda ya Gregory (Christian) na julian.
UTANGULIZI
The date of birth of Jesus of Nazareth is not stated in the gospels or in any secular text, but most scholars assume a date of birth between 6 BC and 4 BC.Two main methods have been used to estimate the year of the birth of Jesus: one based on the accounts of his birth in the gospels with reference to King Herod's reign, and another based on subtracting his stated age of "about 30 years" from the time when he began preaching (Luke 3:23) in "the fifteenth year of the preaching
Luka 3:1 Mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake kaisari tiberio...]
Kaisari Tiberio alimfuata kaisari Augusto katika utawala wa kirumi mnamo Tarehe 19/8/14 BK. Mwaka huo wa 15 wa kaisari tiberio ni kitambo toka tarehe 19/8/28 mpaka tarehe 18/8/29. Hivyo Yesu katika mwaka huo wa 15 alikua na miaka therathini na tatu au hata 36.
Jinsi Dioniso alivyoweka mwaka wa Yesu.
Katitka 3:23 Mwinjili luka aliandika kua Yesu alipoanza kuhubiri alikua na miaka 30 hivyo sasa mnamo karne ya 6 Dioniso alitumia tarakimu hiyo 30 kama msingi wake kua Yesu kipindi iko alikua na miaka 30.
Lakini mwinjili mwenyewe anasema umri wa Yesu ulikua kati ya miaka 30 kwahiyo mwaka aliobuni Dioniso kama mwaka wa kuzaliwa kwake Yesu amepitwa miaka mitano au zaidi. Herode mkubwa aliyetaka kumwua Yesu amekufa mwaka wa nne kabla ya tarehe ya kuzaliwa Yesu iliyobuniwa na Dioniso. Kwahiyo Yesu kazaliwa kitambo kidogo kabla ya kufa herode , hivyo ukijumlisha miaka hiyo 5 na kitambo hiko kidogo twapata kama miaka 7. Kwahiyo tarehe ya kuzaliwa Yesu ni kati ya miaka 5 hadi 7 kabla ya tarehe iliyobuniwa na Dioniso. Kwaiyo inawezekana pia Yesu aiishi miaka zadi ya 33.
Wafahamu chimbuko la Maherode
Wakuu Wayahudi tangu walipodai watawaliwe na wafalme ukirejea 1sam 8:1-9,Mungu aliruhusu wafalme wawatawale wakianzia na Saul, Daud na baadaye Sulemani.Hawa wote walianza kazi zao vizuri lakini polepole mwishoni mwa kazi zao hawakuweza kuendelea kuyashika maagizo ya Bwana na hivyo wakalifanya taifa zima kupotea njia.Mambo kama haya ndiyo hatimaye yanawapeleka waisrael utumwani mnamo mwaka 587 KK.
Ilipofika mwaka 63 KK nchi ya wayahudi ikiwa chini ya utawala wa Aristobulus II, ilitekwa na warumi waliokuwa wakiongozwa na Pompey.Warumi hawa waliitawala nchi ya wayahudi kutoka Roma.Wafalme walioitwa Makaisari walikaa Roma na nchi zote walizoziteka walizigawa katika mikoa ambayo iliwekwa chini ya magavana. Hawa magavana waliweka wafalme wa kienyeji. Kumbe, hawa wafalme wa kienyeji walitawala chini ya gavana wa kirumi.Ni kama kwa mfano jinsi wakoloni hapa nchini kwetu walivyoteua machifu kuongoza badala yao enzi za ukoloni.Hapa naweza kukutajia magavana wachache kati ya wengi wanaojulikana kama Ponsio Pilato,Titus,Felix,Festus n.k
Kumbe jina Herode ni jina la ukoo uliotawala nchi ya Palestina kwa muda wa miaka 47 kabla ya Kristo na miaka 79 baada ya kuzaliwa Kristo.Hawa niliowataja walikuwa wafalme wa kienyeji waliowekwa kutawala badala ya Warumi na kwa kweli hao ndio waliotumia jina Herode.
Pia, watawala hawa yaani maherode, walitoka katika shina moja yaani baba yao alikuwa anaitwa Antipater mtawala wa Idumea, kusini mwa nchi ya Palestina ambaye alikuwa amechaguliwa na Warumi kutawala eneo hilo. Huyu alipata kuzaa mtoto mmoja anayejulikana kama Herode Mkubwa.Huyu Herode Mkubwa,alipewa nafasi ya kutoka katika nchi yake kuja Palestina kwa Wayahudi na kutawala katika mkoa wa Galilaya baada ya kifo cha baba yake na ingawa mwenyewe hakuwa myahudi akatawala tangu mwaka 37-4KK.Wayahudi hawakumpenda mtu huyu kutokana na sababu mbili kuu. Kwanza ni kwa sababu hakuwa myahudi hivyo walijisikia vibaya kutawaliwa na mtu ambaye hakutoka katika taifa lao. Sababu ya pili ya kutompenda ni kwamba Herode huyu alikuwa ni katili sana. Ukatili huu unatokana na ukweli kwamba aliyapata madaraka kwa ujanja. Herode huyu alijua kwamba wengi hawampendi hivyo akajitahidi kuhakikisha kuwa wote wanaompinga anawaangamiza rej Lk 19:27.Tunaambiwa kwamba aliwaua hata ndugu zake na watoto wake mfano akina Antipater, Alexander na Aristobulus walioonekana vinara wa kumpinga. Ukisoma pia Mt 2:16-18 pale wanatajwa watoto mashahidi waliouawa katika harakati za kuhakikisha kwamba mtoto Yesu anauawa pia ingawa hakufanikiwa kumuua Yesu kwani tayari alikuwa ametoroshwa toka Bethlehemu.
Kila mtu anayo mazuri na mapungufu. Herode Mkubwa naye kafanya kitu fulani ambacho kiliwafurahisha Wayahudi pamoja na ukatili wake.Yeye ndiye aliyejenga hekalu la Yerusalemu,hekalu lililokuwa kubwa na zuri kiasi kwamba wayahudi hao hao wakawa wanasema kwamba kama mtu alizaliwa hadi akafa bila kuliona hekalu lile,basi mtu huyo atambue kwamba hakuwahi kuona kitu chochote kizuri hapa duniani.Kumbe huyo ndiye Herode aliyetishia maisha ya Yesu maana hakupenda aje mtu yeyote atakayeitwa mfalme tofauti na yeye.Aliposikia kwamba amezaliwa mtoto ambaye ni mfalme alijua mtoto huyo anataka kurithi ufalme wake hivyo alifanya lolote awezalo ili kuhakikisha anammaliza bila kujua kwamba ufalme wa mtoto Yesu haukuwa wa kidunia.
Herode Mkubwa naye alikuwa na watoto. Kabla ya kifo chake aliacha wosia ulioagiza kwamba nchi aliyoitawala igawiwe kati ya watoto wake watatu yaani Archelaus, Herod Antipas na Philip.
Katika mgao huo, Archelaus akawa mtawala wa Yudea na Samaria na kwa kweli hii ni karibu nusu ya nchi yote ya wayahudi kwani alitawala mikoa miwili. Herode huyu ndiye alikuwa mtawala kipindi kile Yoseph na Maria waliporudi kutoka Misri rej Mt 2:22.Hata hivyo alishindwa kumudu uongozi wa mikoa hiyo na hivyo Warumi wakamtoa na kumweka Pontio Pilato kuwa mtawala badala yao. Mtoto wa pili yaani Herode Antipas alipewa kutawala mkoa wa Galilaya tangu mwaka 4KK-39 BK.Huyu alitawala wakati Yesu alipokuwa akitembea huko na huko kuhubiri Lk 3:1,MK 6:4 Zaidi sana,huyu ndiye Herode aliyekemewa na Yohane Mbatizaji alipomwoa Herodia mke wa kaka yake Philip rej Mt 14:1-5,Mk 6:14-29,ndiye anayeitwa na Yesu mbweha Lk 3:32,na Ndiye aliyekutana na Yesu wakati wa mateso Lk 23:7-12. na mwisho ndiye aliyemuua mtume Yakobo na kumfunga mtume Petro Mdo 12:1-5.
Da'Vinci
Comments
Post a Comment